Kurudiarudia kuimba na kutafakari pamoja kunamuamsha Kundalini. Kundalini ni nguvu ya mungu wa kike ambayo imelala tuli katika namna isiyoonekana chini ya uti wa mgongo katika mwili wa binadamu. Ameunganishwa kwenye viungo sita vya nguvu isiyoonekana iitwayo Chakras iliyowekwa juu ya nyingine katika uti wa mgongo. Wakati Siddha Guru (Bwana mkamilifu) kama vile Guru Siyag anapomuamsha Kundalini kwa kutoa Shaktipāta (kumpa nguvu ya kiroho) kwa sala yake ya kiungu, anajitokeza kupitia chakras sita na hatimaye anafikia Sahasrara, sehemu katika taji la kichwa, ambapo Mungu anakaa. Kundalini aliyeamshwa hutakasa mwili mzima wa mwombaji kwa kuleta āsanans za bila hiari za yoga kriyās, bandhs, mudras, Pranayam na kadhalika wakati wa kutafakari. Mwombaji hawezi kuanzisha au kusitisha mihemko hii ya Yoga kwa hiari na akili yake mwenyewe. Hizi Kriyās humwondoa mwombaji kutoka katika taabu za mwili na akili, ulevi, na humtia katika Moksha kwa kumweka katika njia ya mabadiliko ya kiroho.