Kila mtu ana tabia tatu za asili: Sāttavic (safi, nyepesi), Rajasic (shauku) na Tamasic (kuzubaa, uzembe). Tabia hizi huamua si tu kupona kwa jumla kwa akili ya mtu, mtazamo juu ya maisha na matendo, bali pia upendeleo wake wa mlo au au uchaguzi wa vyakula na vinywaji atakavyotumia. Mazoezi ya mara kwa mara ya GSY huwezesha utawala wa Sāttavic kuliko Rājasic na tabia za Tāmasic , na hivyo kusababisha mabadiliko yanayohusiana na tabia mbili zinazofuatia. Utawala kwa ubora wa Sattvic kwa upande mwingine huleta mwelekeo wa tabia za mtu za ndani kuelekea matendo mazuri ya ufahamu, akili na kufikiria kwa sahihi. Ndivyo inavyokuwa pia kwa upendeleo wake wa chakula na vinywaji. Matokeo ya jumla ya mabadiliko haya ni kwamba chochote ambacho ni kibaya na chenye madhara kwa ustawi wa mwili na akili ya mtu na mageuzi ya kiroho humuacha kwa hiari yake mwenyewe bila juhudi ya ufahamu wa mtu kufanya hili kutokea. Hivyo, kama mtu anasumbuliwa na ulevi wa madawa, pombe au kuvuta sigara, ulevi au kuzoelea madawa kutamwacha au kama anapendelea aina ya chakula ambacho kina madhara kwa afya yake, atapiga hatua ya kukichukia taratibu na kurejea kwenye maamuzi mazuri ya kiafya kwa sababu ya mabadiliko katika sifa na tabia yake ya ndani kulikoletwa na kuiimba kwa mantra na kutafakari. Swami Vivekanand amesema kuhusu kuondokana huku kwenyewe kwa ulevi, “Huhitaji kuacha/kuondokana na vitu; vitu vyenyewe vitakuacha/vitaondokana nawe.