• Kaa katika mkao wa kutulia.
  • Unaweza kukaa kwa kukunja miguu sakafuni, lala chini, kaa kwenye kiti / kochi n.k., ili kutafakari.
  • Angalia picha Guru Siyag kwa dakika moja au mbili hadi ukumbuke picha.
  • Kisha funga macho yako na zungumza kimykimya kwa Guru Siyag, “Nisaidie kutafakari kwa dakika 15.”
  • Kisha, na macho yako yakiwa bado yamefumbwa, fikiria picha ya Guru Siyag kati sehemu kati ya nyusi zako (pia inajulikana kama jicho la tatu). Hii ina maana kwamba unatakiwa ujaribu kufikiria picha ya Guru Siyag katika akili yako katika sehemu ya paji la uso.
  • Wakati unafikiria picha, rudia kimyakimya (kuimba) kwa dakika 15 mantra (maneno ya sala ya imani) iliyotolewa na Guru Siyag. (Angalia ‘Jinsi ya kupokea Mantra)
  • Wakati wa kutafakari, unaweza kuona mikao ya yoga ya ghafla bila hiari au mishtuko. Kuyumba, kutikisika kichwa, kucheza kichwa kwa kasi kutoka kushoto kwenda kulia na kushoto tena, kutanuka/kujaa hewa na kunywea kwa tumbo, kupiga makofi, kuunguruma, kunung’unika au kucheka kunaweza kutokea mara nyingi. Usipaniki wala kuwa na wasiwasi.  Hatua hizi zinatokea ghafla bila kutaka, zimepangwa na nguvu ya Mungu Kundalini, na zinahitajika kwa ajili ya kukutakasa ndani na kukuweka tayari kwa ajili ya hatua zaidi nyingine.
  • Unaweza pia kuona mitetemo, kuona mwanga mkali, rangi au hata kuwa na maono au ishara za siku za nyuma na matukio ya baadaye. Hizi ni dalili kwamba unaendelea vizuri katika njia ya kiroho.
  • Hata hivyo, hata kama hauoni mikao yoyote ya yoga au hauoni maono, haimaanishi kwamba hauendelei. Kwa uwezekano wote, nguvu ya Mungu iliyoamshwa ndani yako labda imeamua kwamba hauhitaji hali hizi.
  • Utaona kwamba kutafakari kwako kutafikia mwisho hasa utakapofikia kikomo cha wakati uliokuwa umeweka awali.
error: Content is protected !!