- GSY inatokana na Ashtanga yaani falsafa ya (viungo vinane/miguu minane) ya Yoga kama ilivyopangiliwa na Sage Patanjali katika Yoga Sutra. Mazoezi ya GSY hupelekea katika utambuzi rahisi usiohitaji nguvu wa viungo hivi vinane.
- Baada ya mazoezi endelevu, uimbaji wa mantra (marudio akilini) unakuwa/unafanyika wenyewe bila hiari. Hali hii hujulikana kama Ajapā Japa. Katika hali hii, mwombaji/mtendaji anaona kuwa mantra yaani maneno ya sala ya kiungu yanaimbwa bila ukomo ndani ya yake yenyewe bila hiari yake mwenyewe, bila yeye kuamua kwa upande wa mwombaji/mtendaji.
- Wakati mwombaji anapoimba maneno haya ya sala ya kiungu ya mantra bila kuchoka (au anapoona Ajapā Japa), yanajibadili yenyewe kuwa katika sauti ya kiungu. Hii inajulikana kama Anhad Nada. Sauti halisi ya umbo inatengenezwa wakati kitu kimoja kinapogonga kingine. Hii sauti ya mbinguni haina asili hiyo ya umbo; haigongwi, ni sauti isiyokoma ambayo inaenea ulimwengu mzima. Nad inasikiwa na mwombaji katika moja ya masikio yake, na ni dalili ya mwombaji kuvuka kizingiti kikuu cha hatua za kiroho.
- Kwa njia ya mazoezi ya GSY, mwombaji anapata nguvu nyingi za kiungu. Moja ya nguvu hizi za kiungu inajulikana kama Prātibh Gyāna (Maarifa ya kung’amua bila kufikiri sana). Wakati maarifa haya yanapopatikana, mwombaji anaweza kutabiri na kusikia matukio ya siku zijazo yasiyo na ukomo na pia ana maono ya siku za nyuma.
- Wakati wa kutafakari, waombaji wanaweza kuona Khechri Mudra, mkao wa kiYoga ambapo ulimi unavutwa nyuma na unachoma sehemu ya juu ya kinywa ambayo inatoa Amrit, nekta/asali ya miungu, ambayo ni dawa ya maji ya maisha uishi muda mrefu ukiwa kijana. Amrit inaimarisha kinga ya mwili na inamwondoa mwombaji katika magonjwa yasiyotibika.
- Mazoezi ya GSY huleta mabadiliko katika Vrittis (tabia za ndani) za mwombaji kutoka Tāmasic (giza, kuzubaa, uzembe) kwenda Rājasic (shauku, kuchangamka) ili kuwa Sāttavic (mwenye bidii, msafi, mwelewa). Mabadiliko katika Vrittis kimsingi yana maana ya mabadiliko kwa ujumla katika nafsi/utu wa mwombaji.
- Mwombaji hatimaye anafikia hatua ya Moksha (uhuru wa kutoka katika mzunguko wa maisha na kifo) na mabadiliko ya kiungu.
error: Content is protected !!