Sayansi ya Tiba inatibu msongo kwa madawa ya kuzoelea/kulevya (dawa za kutuliza kwa kulala, vidonge vya usingizi, dawa za kuzuia hali fulani n.k.) ambazo kwa nadra zina uwezo wa kutibu mgonjwa. GSY pia inaona ulevi kama tiba lakini ni aina ya kulevya Ananda (furaha au neema) inayoletwa na kuimba mara kwa mara kwa maneno ya sala ya kiungu yaani mantra ya Guru Siyag. Wahenga wameelezea neema hii ya kiungu kama “ulevi bila madawa ya kulevya.” Ananda humwondoa mwombaji katika msongo na magonjwa yanayohusiana na msongo kama vile huzuni, shinikizo la damu, kukosa usingizi, hofu ya kitu, n.k. kwa siku chache tu.